Waraka wa Shikh Mohammedi Iddy kuhusu umuhimu wa Mahakama ya Kadhi itakayotoa suluhu kwenye kesi za ndoa za dini ya kiislam.
Sheikh Iddy ameeleza kuwa Mahakama zilizokuwepo hazina uwelediwa kusuhisha masuala ya ndoa za kiislam kutokana na kuibua migongano.
amesema kuwa Mahakama hiyo haihalibu utaratibu wowote wa kidola kama ilivyo Zanzibar , na kukosekana kumewaathiri waislam kwenye migogoro ya ya ndoa hizo kutokana na Makadhi waliokuwepo hawana Mamlaka kamili kisheria.
Sheikh Iddy ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya kiislamu ya alsara amesisitiza kuonana na Profesa Palamaganda Kabudi Waziri wa Sheria na Katiba ili kumueleza umuhimu na athari za utokuwepo kwa Mahakama hiyo kwa Waislamu
zinazohusiana na masuala ya diniHivi karibuni kupitia Jamhuri ya muungano wa Tanzania tumemsikia Mheshimiwa waziri wa sheria na Katiba Profesa Palamaganda Kabudi akitoa nasaha alisema (nanukuu).
“….Mashauri ya ndoa mashauri ya mirathi mashauri yanayogusa yanayogusa mila na desturi mashauri yanayogusa dini , ni vyma tukayaendea kwa uangalifu mkubwa . Na niseme kwa unyenyekevu mkubwa soma hili la ndoa nimelindisha kwa miaka kumi na tisa sio eneo jepesi”
Maneno hayo ya Mheshimiwa waziri Kabudi yanaamaanisha mambo makuu mawili kwanza anatuthibitishia kwamba yapo matatizo au kero nyingi katika masuala ya sheria ya ndoa na masuala ya dini.
Pili anatunasihi tuwe na umakini mkubwa katika kuyatafutia ufumbuzi matatizo au kero hizo.
Kupitia Taarifa hiyo ya Mheshimiwa Waziri Kabudi nimeonelea nimsahuri kwamba njia mojawapo ya Kuindea katika kuyatatua matatizo hayo ni urejeshwaji wa Mahakama ya Kadhi .
Ni vizuri Nikukumbusha Mheshimiwa Waziri kwamba maombi ya Waislamu wa Tanzania bara kutaka kurejeshwa Mahakama ya Kadhi sio jambo jipya na tayari limeshapitia michakato kadhaa lakini kwa sababu haikuwepo dhamira ya dhati kwa serikali kuwarejeshea waislamu Mahakama hiyo mafanikio hayakufikiwa.
Mheshimiwa waziri anakumbuka mengi jii ya kadhia ya Mahakama hiyo lakini kamwe hawezi kusahau kwmaba bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania liliwahi kuunda tume ya kibunge nchini ya uenyekiti wa Mheshimiwa Athumani Jenguo aliyekuwa mbunge wa jimbo la kisarawe Mkoani Pwani.
Tume hiyo ilihoji na kujiridhisha juu ya hitajio la waislamu kurejeshewa Mahakama ya Kadhi lakini ripoti hiyo haikusomwa bungeni kama tulivyozoea kuona ripoti za kamati na tume mbalimbali za kibunge.
Juhudi za mchakato wa kuifanyia marekebisho sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ili sheria hiyo izitambue hukumu zitakazotolewa na Makadhi hawa wasiokuwa na meno ( wasiotambuliwa na sheria za nchi) zilikwamishwa kwa kusitishwa mchakato huo.
Ukweli ni Kwamba hakuna njia ya mkato katika kutatua migogoro inayotokana na sheria ya ndoa ya mwaka 1971 zaidi ya kufunya mojawapo kati mambo yafuatayo:-
Kurejesha Mahakama ya Kadhi yenye meno yake Kamili,. Pili kuifanyia marekebisho sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ili kiwepo kipengele kitakachotambua hukumu zinazotolewa na Makadhi hawa waliopo sasa , tatu sheria ya ndoa ya mwaka 1971 itambue ndoa ya kiislamu kwa ujumla wake na ukamilifu wake kwa maana itambue kufungishwa kwake , maisha yake , takaka yake, rejea yake , eda yake na kadhalika.
Nina hakika kwamba Mheshimiwa Waziri Kabudi ambaye amekiri kusomesha somo la ndoa kwa takribani miaka 19 anafahamu zawi migongano iliyopo katika ya matakwa ya sheria ya ndoa ya mwkaa 1971 na usahihi wa ssheria ya ndoa ya kiislamu.
Mifano michache:-
Sheria ya kiislamu katika ufungishaji wa ndoa inahitaji kuwepo kwa walii( mfungishaji ndoa) ambaye huwa ni Baba , Babu , Kaka na kadhalika (mtu yoyote atakayefungisha ndoa ukimuondoa walii atakuwa amewakili8sha walii wakati sheria ya mwaka 1971 inamtambua sheikh mwenye leseni kuwa ndiye mfungishaji ndoa wala haimtambui Baba kama mhusika mkuu.
Sheria ya ndoa ya kiislamu hailazimishi kuwa ndoa ili iwe halali ifanywe maeneo ya wazi bali kuitangaza ndoa ni Sunnah, (Jambo jema lenye malipo kwa mungu) . Lakini Sheria ya mwaka 1971 inalazimisha suala la uwazi katika kufunga ndoa.
Sheria ya ndoa ya kiislamu inampa walii (Baba na kadhalika) nguvu ya kukataa bint yake asiolewe na mwanaume wa dini nyengine kwa kuwa ndoa hiyo sio halali na waliooanana kwa ndoa hiyo watahesabiwa ni wazinifu kama wazinifu wengine katika jamii,. Lakini kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka 1971 inaona na kuitambua nddoa hiyo kuwa sahihi haswa baada kutolewa tangazo la kusudio la ndoa na kukosekana pingamizi lolote kuzuia kusudio hilo.
Huo ni Mgongano kati sheria ya ndoa ya Mwaka 1971 na matakwa ya sheria ya ndoa ya kiilsamu kwa upande wa kufunga ndoa kwa upande wa talaka ni kama ifuatavyo:-
Talaka anayoitoa Muislam inatosha kuvunja ndoakwa muijbu wa sheria ya ndoa ya kiislam . wakati talaka kwa upande wa sheria ya ndoa ya mwaka 1971 haipati uzito wa sheria mpka kipatikane cheti cha mahakama kinachothibitisha kuvunjika kwa ndoa hiyo, kwa mukatadha huo muislamu hana uwezo wa kutoa talaka yake ikatambulika kisheria kwani talaka anayoitoa muislam inahesabika kuwa ni kusudio la kuivunja ndoa.
Aidha hiyo talaka ya muislam ambayo sheria ya ndoa ya mwaka 1971 haitambui mpaka ithibitishwe na mahakama katika uislam imegawanyika katika makundi kadhaa ambayo hiyo Mahakama ya nchi na mahikimu wake hawawezi kuzitambua wala kujua kinachozaliwa baada ya talaka hizo.
Zipoa aina nyingi za takala ikiwa pamoja na ile Talaka ya Wazi (Twalaq Swarih), Talaka ya fumbo (Twalaq Kinaahah)ipo talaka nya kujivua (Khul-i) na Talaka ambayo Mwanandoa mmoja akibadilisha dini basi ndoa inavunjiaka bila kutolewa au kutamkwa ka watalaka na kadhalika.
Kwa uchambuzi huo Mheshimiwa Kabudi ataanguna na mimi kwamba ndoa na talaka katika uislam ni jambo kubwa na pana linalohitajia mahakimu maalum wenye utaalamu usiotiliwa shaka.
Naomba nitumie fursa hii kumuomba Mheshimiwa Waziri Kabudi kwa kuzingatia kwamba katika wakati huu amabpo yeye ni waziri wa sheria na Katiba Mwalimu wa sheria na Mtaalamu katika somo la ndoa alilofundishwa kwa miaka 19 naamini ndio
