Polisi yamnasa Jambazi anayetumia mavazi ya kijeshi


Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linamshikilia Erick Francis Chilemba (30) muhudumu wa  hotel ya Sleep Inn na Mkazi wa Mwanayamala kwa Kopa kwa tuhuma za kukutwa na sare za Jeshi la Polisi, silaha, cheo cha koplo, pingu na nguo nyingine inayofanana na sare za JWTZ.

Hayo yameelezwa na kamanda wa jèshi hilo Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa,  Jeshi la Polisi lilipokea taarifa kutoka kwa msiri kuwa kuna mtu mmoja  anatumia sare za Jeshi la Polisi kuwakamata watu na kuwafunga pingu, kuwatishia bastola ili kufanikisha  kupora mali maeneo mbalimbali ya Jiji.

Baada ya kupata taarifa hizo Jeshi la Polisi lilianza ufuatiliaji mara moja na kuweka mtego.
 Mnamo tarehe 12 Mei 2018 majira ya saa nne usiku huko Mwenge Bamaga Polisi  walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo.

Baada ya kufanya naye mahojiano mtumiwa alikiri kumiliki sare na vifaa mbalimbali vya Jeshi la Polisi na kukubali kuwapeleka askari hadi nyumba anayoishi na baada ya kufanya upekuzi kwenye nyumba hiyo alikutwa na sare za Jeshi la Polisi, pingu, cheo cha koplo wa Polisi, mfuko wa kuhifadhia bastola na bastola aina ya GLOCK 17 ambayo imefutwa namba zake za usajili ikiwa haina risasi.

Mtuhumiwa huyo ameshafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Post a Comment

Previous Post Next Post