Mlinda mlango wa klabu ya Liverpool, Loris Karius amekubali kubeba lawama ya kukosa ubingwa wa Champion League baada ya timu yake kukubali kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya mabingwa wa ligi hiyo Real Madrid.
Mlinda mlango huyo amekiri kwamba alifanya makosa makubwa
mawili yaliyozaa magoli hayo katika mchezo wa fainali uliopigwa jana, na
kuepelekea Real Madrid kutwaa ubingwa.
Makosa hayo ni pamoja na kuipa mwanya Real Madrid wa kupata
bao la kuongoza katika dakika ya 51 kupitia mshambuliaji wake Karim Benzema.
Karius alifanya kosa hilo alipojaribu kuharakisha kuanzisha mashambulizi ambapo
alirusha mpira mbele ya Benzema.
Karius amewaomba msamaha mashabiki wa Liverpool kutokana na
makosa hayo yaliyoigharimu klabu hiyo kukosa ubingwa.
"Naomba
samahani kwa kila mtu, kwa timu, kwa klabu ,
kwamba makosa hayo yameigharimu timu. Iwapo
ningerudisha nyuma muda , ningeweza. Nina masikitiko
makubwa kwa timu yangu. Nafahamu nimewaangusha
leo. Magoli haya yametugharimu kukosa ushindi,
kimsingi," alisema.
