Aliyekuwepo kwenye Kontena Zanzibar apatikana ...hiki hapa kisha chake


Hassan Juma Hassan 36, mkaazi wa Miembeni mjini Unguja, a,emenusurika kufa baada yakufungiwa ndani ya kontena kwa siku nne baada ya yeye kuchukuliwa na usingizi mzito kiasi cha kontena hilo kuhamishwa bila ya yeye kujitambuwa.

Juhudi zake zakujiokowa ziligonga mwamba baada ya kontena hilo kuhamishiwa sehemu yenye mbanano wa makontena mengine kiasi cha sauti kutosikika hadi leo alipofanikiwa kuokolewa baada yakusikika akigonga wakati kontena hilo likihamishiwa sehemu nyingine.

Kwasasa amelazwa kwenye hospitali kuu ya Mnazi mmoja huku ikielezwa kwamba hali yake inaendelea vizuri.

Post a Comment

Previous Post Next Post