Vijana wa ACT-Wazalendo waishukia Bodi ya Mikopo

Ngome ya Vijana wa chama cha ACT-Wazalendo leo Jumamosi Mei 13, 2018 imejitokeza na kuendeleza mjadala wa kipengele chenye utata kwenye Mwongozo wa uombwaji wa mikopo uliotolewa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).

Vijana hao wameitaka HESLB kufanya marekebisho katika kipengele ambacho kinadaiwa kuzuia wanafunzi wenye wazazi ambao wanamiliki biashara hawataruhusiwa kuomba mikopo.

Mwenyekiti wa Ngome hiyo, Likapo Bakari Likapo amesema kuwa kipengele hicho ambacho cha kwanza, sehemu ya saba ya mwongozo huo kinapaswa kuondolewa kwenye tovuti ya Bodi ya Mikopo.

Likapo amesema Serikali imepinga kuwepo kwa kipengele hicho lakini kimeendelea kuwepo kwenye tovuti ya Bodi ya mikopo hivyo kitolewe ili ukanusho wa serikali umaanishe.

"Baada ya watu kupiga kelele kwenye mitandao na kwingine, tukamsikia hata Waziri anasema 'tulikuwa tunawalenga watu wakubwa' lakini watoe hiki kipengele ili ionekane nikweli wamekanusha na wakimaanisha," amesema Likapo.

Post a Comment

Previous Post Next Post