Kishindo cha Joseph
Mbilinyi (Sugu) Mbunge
wa Mbeya Mjini (Chadema), kimesimamisha shughuli za Bunge kwa muda wa dakika takribani
6 ikiwa ni mapokezi yake ndani ya bunge kwa mara ya kwanza tangu atoke gerezani.
Sugu aliiachiwa huru
kutoka magereza terehe 10 Mei Mwaka huu kwa msamaha wa Rais John Magufuli. Leo
kwa mara ya kwanza ameingia bungeni akiwa na mbunge Viti Maalum Kuntu Yusuph (Chadema).
Wabunge wa upinzani
walisherehekea ujio wa Mbunge huyo huku wakigonga meza kwa
furaha wakimshangilia kwa kishindo cha dakika 3.
Wakati huo, naibu waziri wa Tamisemi, Josephat
Kandege aliyekuwa anajibu maswali ya wabunge, alikaa kimya kwa muda kupisha
mapokezi ya mbunge huyo.
Alitinga na nyeusi suti
ambapo upande wa kushoto kuna nembo inayoonyesha namba ya mfungwa yenye taarifa
za kifungo alichotumikia .
Sugu aliingia ndani
na kuanza kuwasilimia wabunge kwa kuwa mikono aliianza kwa Nape Nnauye Mbunge
wa mbunge wa Mtama, Nape Nnauye ,Dk Adelardus Kilangi Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), George
Mkuchika akawapa na kumpa mkono kisha kwa Jenister Mhagama waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi na Watu wenye Ulemavu.
Sugu alielekea upande
walioketi wabunge wa upinzani na kukumbatiana na mbunge wa Rombo (Chadema),
Joseph Selasini na kwenda kukaa sehemu yake karibu na mbunge wa Tarime Mjini
(Chadema), Esther Matiko.
Andrew Chenge ,Mwenyekiti
wa Bunge aliwaomba wabunge kutulia ili shughuli za Bunge ziendelee, huku
akiwatishia kuwa hatawapa nafasi ya kuuliza maswali ya nyongeza.
“Imetosha sasa,
imetosha, haya endelea,” amesema Chenge
