Trump atishia kujiondoa katika mazungumzo na Kim Jong-Un

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa iwapo mazungumzo yake na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un hayatazaa matunda 'ataondoka katika mazungumzo hayo'.
Trump ameyasema hayo huku akithibitisha ukweli wa kuwa Mkurugenzi wa CIA nchini humo, Mike Pompeo siku za nyuma alifanya ziara ya kisiri kwenda Korea Kaskazini  kuweka mazingira ya yeye kukutana na Kim Jong Un.
Akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari Trump amesema yeye na waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe wanadai ya kuwa shinikizo lao dhidi ya Korea Kaskazini ni sharti iendelee kwa kukataa kusitisha utengezaji wa silaha za nyuklia.
Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe amewasili leo katika mgahawa wa rais Trump wa Mar-a-Lago resort mjini Florida kwa mazungumzo.
Trump amesema kuwa Pompeo ameweka uhusiano mzuri na Kim ambaye alimwita 'bwana mdogo' na kwamba mkutano wao ulifanyika vizuri.
Ziara hiyo iliadhimisha mawasiliano ya juu kati ya Marekani na Korea Kaskazini tangu 2000.
Mkutano kati ya Trump na Kim unatarajiwa kufanyika kufikia mwezi Juni huku eneo litakalofanyika mkutano huo bado yanaendelea kufanyiwa kazi.

Post a Comment

Previous Post Next Post