Na Mwandishi wetu, 24SevenUpdater
Mwanamuziki nguli wa muziki wa dansi nchini, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na watoto wake Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ na Francis Nguza, leo Alhamisi ya Aprili 19, 2018 wametembelea Bungeni Dodoma baada ya kualikwa.
Familia hiyo ya mwanamuziki Babu Seya ilifika bungeni hapo kwa mwaliko wa Mbunge wa Viti Maalum CCM, Mariam Ditopile ambapo walishangiliwa na wabunge baada ya kutambulishwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Hayo yamefanyika baada ya kipindi cha maswali na majibu kumalizika bungeni humo.
Wanamuziki hao walikuwa ni miongoni mwa wafungwa 8,157 waliosamehewa na Rais John Magufuli siku ya maadhimisho ya sherehe za Uhuru wa Tanganyika, Desemba 9, 2017 zilizofanyika mjini Dodoma.
