Na Abdul Hussein, 24SevenUpdater
Kituo cha televisheni cha Azam TV kimepewa dhamana ya kurusha matukio yote ya moja kwa moja harusi ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ally Kiba itakayofanyika Kenya na Tanzania baadaye mwaka huu.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram wa Azamtv wameandika "EXCLUSIVE ALIKIBA ANAOA!!! Azam TV ndiyo kituo pekee kitakuletea sherehe ya harusi ya mwanamuziki maarufu @officialalikiba. Tunaanzia Mombasa, tunamalizia Dar es Salaam.
Ali kiba ndiye atakuwa msanii wa kwanza nchini Tanzania kuoneshwa harusi yake moja kwa moja kwenye kituo cha Azam TV kitu ambacho wenzake waliowahi kuowa hawakukifanya
Hata hivyo staa huyo bado hajathibitisha tukio hilo na hii ni kutokana na msani huyo kufanya mambo yake kwa siri tofauti na mastaa wengine
