Wema ana kesi ya kujibu juu ya matumizi ya dawa za kulevya



Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imemkuta na hatia msanii Wema Sepetu na wafanyakzi wake wawili, kwa kosa la matumizi ya madawa ya kulevya.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu, Simba baada ya kupitia ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na mashahidi watano wa upande wa mashtaka waliokuwa wakiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula, na kusema kwamba Wema na wenzake wataanza kujitetea Mei 14 na 15, 2018.

Kabla ya uamuzi huo kutolewa Wakili Kakula aliiambia mahakama kuwa kesi hiyo leo ilipangwa kwa ajili ya uamuzi kama washtakiwa hao wana kesi ya kujibu ama la, na ndipo Hakimu Simba akasema kwa mujibu wa sheria iwapo washtakiwa watapatikana kuwa wana kesi ya kujibu wataanza kujitetea.

Hata hivyo baada ya kupitia hoja zote zilizowasilishwa mahakamani hapo, Hakimu Simba amesema Mahakama imejitosheleza kwamba washtakiwa wote wana kesi ya kujibu katika mashtaka yote, hivyo wana haki ya kisheria kuanza kujitetea.

Wema na wafanyakazi wake wawili wanakabiliwa na kesi ya kutumia madawa ya kulevya aina ya bangi, na kesi hiyo imehairishwa mpaka Mei 14 mwaka huu.


Post a Comment

Previous Post Next Post