Msemaji wa Klabu ya Simba Haji Manara ameseam kuwa atakuwa mtu wa kwanza kutunga wimbo utakao wakutanisha Msanii wa Bongo Flavor Nasibu Abdul (Diamond) na Ali Kiba kwa kuwashirikisha nyota hao.
Manara amesema hayo alipokuwa akizungumzia ushindi wa bao moja wa klabu yake ya simba dhidi ya wapinzani wao wa jadi klabu ya Yanga .
Akizungumza kwa Furaha ya ushindi huo haji manara alisema kuwa leo yupo kwenye furaha hivyo kesho atazungumza mengi.
manara ameeleza kuwa atahudhuria kwenye harusi ya Alikiba inayofanyika usiku wa leo akiwa ametinga kanzu yenye rangi nyekundu yenye kuashiria timu ya simba
