Klabu ya Yanga imeandika ya kujitoa kwenye mashindano Kageme yanayotarakiwa kuanza Juni 28 mwaka huu.
Uongozi wa klabu ya hiyo umewaandikia barua Shirikisho la Mpira wa Miguu nchi TFF kuwaomba kujitoa katika mashindano hayo jana.
Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa Sababu za msinngi zilizofikia Yanga kuandika barua hiyo ni kufanya maandalizi ya michunao ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo watacheza na Gor Mahia FC ya Kenya, Julai 18 jijini Nairobi.
Kutokana na muingiliano wa ratiba ya Kagame na CAF, Yanga wameona ni vema kuwapatia wachezaji wao mapumziko ili kuwapa fursa ya kujiandaa vizuri kuelekea mechi hiyo ambayo itakuwa ni ya tatu baada ya kucheza na USM Alger pia Rayon Sports ya Rwanda.
Wakati huo watani wao wa Jadi Simba SC kupitia msemaji wao Haji Manara ameeleza kuwa kujitoa kwa klabu hiyo n8 ishara ya kuwaogapo na kuwakwepa kwenye mechi inayowakutanisha Julai Saba.
