Mameneja masoko watano kutoka masoko ya Mabibo, Shekilango,
Mahakama ya Ndizi, Simu 2000 na Sinza namba mbili, wamekalia kuti kavu baada ya
Kamati ya fedha ya Manispaa ya Ubungo kuagiza wasimamishwe kazi.
Kamati hiyo imemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, John
Kayombo kuwasimamisha kazi mameneja hao kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za
mapato zaidi ya milioni 200.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Meya wa
Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob amesema ubadhirifu huo umegundulika kufuatia
ukaguzi wa ndani uliofanywa na mkaguzi wa manispaa hiyo.
Amesema fedha hizo ambazo ni kati ya Sh. Bilioni 1
zilizokusanywa katika kipindi cha miezi tisa hazikupelekwa benki.
