Klabu ya Liverpool imefanikiwa kumnasa mchezaji wa Lyon,
Nabil Fekir, ambapo iko katika hatua za mwisho za kusaini nae kwa dau la paundi
milioni 53.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa, alikuwa anawindwa na
kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp katika dirisha la usajili katika msimu wa
majira ya joto.
Kocha Klopp anaamini kwamba Fekir atakua na nafasi nzuri ya kuichezea
klabu hiyo kwa muda mrefu.
