Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania-KKKT na Baraza la
Maaskofu Tanzania-TEC yameombwa na kambi rasmi ya upinzani bungeni kutojibu
barua waliyopewa na serikali hivi karibuni.
Barua hiyo ya serikali ilitoa maagizo kadhaa ikiwemo ya
kuyataka makanisa hayo kufuta waraka wa pasaka ndani ya siku kumi.
Akizungumza na wanahabari bungeni jijini Dodoma leo Juni 7,
2018, Mbunge wa Vunjo, James Mbatia ndiye aliyetoa msimamo wa wabunge wa
upinzani ambapo alisema kuanzia sasa watatumia mbinu mbalimbali ndani na nje ya
bunge kuitaka serikali kutoa majibu ya kina kuhusu maagizo hayo.
Msimamo huo wa wabunge wa upinzani umekuja baada ya Naibu
Spika, DKT. Tulia Ackson kumzuia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutojibu swali
kuhusu agizo la serikali la kuitaka KKKT kufuta waraka wake ndani ya siku kumi.
Mbatia ndiye aliyeanzishja mjadala huo bungeni
katika kipindi cha maswali na majibu aliyetaka kujua ukweli kuhusu barua hizo.
