Chama cha Chadema kimepata pigo baada ya diwani wa kata ya
Mawenzi iliyoko Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Hawa Mushi kufariki dunia
jana Juni 7, 2018.
Mushi alifariki dunia jana majira ya jioni akiwa njiani
kuelekea Hospitali ya Rufaa ya KCMC baada ya kuzidiwa akitokea hospitali ya St.
Joseph.
Taarifa ya kifo hicho imethibitishwa na Mwenyekiti wa
Chadema Kilimanjaro, Joseph Selasini.
Selasini amesema mazishi ya marehemu Mushi yatafanyika kesho
Juni 9, 2018 nyumbani kwa wazazi wake maeneo ya kata ya Rau.
