Vyuo 20 vya Ufundi vimefutiwa usajili wake kutokana na kushindwa kutekeleza taratibu za kusajili vyuo hivyo.
Vyuo hivyo vimefutowa usajili huo leo Juni 8, 2018 na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)
Hayo yameelezwa na Dr. Adolf Rutayuga Kaimu Katibu Mtendaji wa NACTE ambapo amsema kuwa kufungiwa kwa vyuo hivyo ni matokeo ya uchunguzi wa baraza hilo uliofanywa mwezi Julai 2017 mpaka Septemba 2017.
Dk Rutayuga amesema kuwa Vipo vyuo vingne 9 vilivyozuliwa kudahili wanafunzi wapya kwa mwaka wa masomo 2018/19 na vyuo 3 vimesitishwa kutoa program zisizohidhinishwa na Baraza hilo.
Amesema kuwa pazia la kuomba usajili upya endapo watarekebisha matatizo na utaratibu ukafuatwa lipo wazi kwa vyuo hivyo
Katika uchunguzi huo uliofanywa kwa vyuo 458 ambapo 112 vya ualimu na vingine 7 vilivyokutwa haviendelei na shughili za elimu, vyuo 426 vimekidhi vigezo lakini vyuo 32 vimekutwa na mapungufu hivyo Baraza limechukua hatua mbalimbali kwa vyuo hivyo 32," amesema.
