Kikosi cha Simba kikifanikiwa kutwaa ushindi kwenye fainali ya michuano ya SportPesa itakayochezwa kesho Jumapili Juni 10 dhidi ya Gor Mahia.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2017/18 wataelekea nchini Italia kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi wakimaliza kibarua chao kwenye uwanja wa Afraha mjini Nakuru.
Simba walitinga hatua huyo baada ya kuwaondosha Kakamega HomeBoyz kutoka Kenya na Gor Mahia wakiiondoa Singida United ya Tanzania.
Fainali ya mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na wadau wengi wa soka la Tanzania na Kenya utaanza majira ya saa 9:00 alasiri
