Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam nchi imembadilishia kifungo Msanii wa Film Nchini Elizabeth Micheal (Lulu) kutoka kwenye kifungo cha Magereza na kutumikia kifungo cha nje.
Novemba 13 mwaka 2017 Lulu alihukumiwa kwenda jela miaka miwili baada ya kukutwa na hatia ya kumuua msanii Mwenzake Steven Kanumba bila kukusudia.
Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Sam Rumanyika baada ya kusikiliza ushahidi wa utetezi na ule wa Jamhuri.
Jeshi la Magereza limethibitisha kupokea amri ya mabadiliko adhabu ya msanii huyo ambapo atatolewa kutoka magereza na ataanza utaratibu wa adhabu yabkifungo cha nje.
