Serikali ya Burundi imepiga marufuku Matangazo ya Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC na ya Sauti ya Amerika, (VOA)
Uamuzi huo ulitolewa na Baraza la Habari la Burundi na kuifunga minara ya vituo hivyo.
Akizungumza Karenga Ramadhani Mwenyekiti wa baraza hilo ameeweka wazi kuwa wamechukua hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko ya Serikali juu tuhuma za uchochezi waliodai kufanywa na idhaa hizo.
Ramadhani amesema kuwa vituo hivyo vimekuwa vikienda kinyume na sheria za utangazaji za ndani na zile za kimataifa.
