Mamia ya wakazi wa Jimbo la Buyungu wilayani Kankonko mkoani
Kigoma wamejitokeza katika shughuli ya mwisho ya kuuaga mwili wa aliyekuwa
mbunge wa jimbo hilo, Kasuku Bilago.
Vile vile shughuli hiyo imehudhuriwa na wanasiasa mbalimbali
ikiwemo Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo,
Zitto Kabwe. 
 



