Zoezi hilo limefanyika Vigwaza, wilayani Kibaha mkoani
Pwani ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Elimu na Mafunzo wa Kikosi cha Usalama
barabarani Tanzania, Abel Swai amesema mara kadhaa wamekuwa wakijitokeza
madereva kulalamika kuwa wanakamatwa kwa kutumia tochi hizo kwa spidi ambazo
sio za kweli lakini matokeo ya uhakiki wa vipimo hivyo yanaonesha kuwa havina
tatizo.
“Hii tuliofanya leo ni kuwaambia wananchi kuwa vifaa hivi
vipoje kama wakala wa vipimo wamejiridhisha maana yake ni sahihi hivyo
pasitokee mtu akalalamika kuna wakati mwingine wanakamatwa kwa spidi sio za kwao,”
amesema Kamanda Swai.
Aidha Mkurugenzi wa Ufundi wa Wakala wa Vipimo wa Serikali,
Stella Kawa, amesema tochi zote zilizohakikiwa zote zinapima vizuri.
“Ukiambiwa ni km 80 au km 70 basi ni 70 kweli, tunawaambia
watumiaji wa magari kwamba unapohisi una wasiwasi na vifaa hivyo basi wafanye
mawasiliano na wakala wa vipimo kwa msaada zaidi.