Vifo vya kina Mama vimeripotiwa kupungua


Vifo vya kina Mama vimeripotiwa kupungua kwa Asilimia 44 ulimwenguni ambapo tangu mikakati ya Kupunguza vifo ilipoanza Miaka 25 iliyopita (1990 -2015) Kumekuwa na Mafanikio Makubwa katika Kupunguza vifo vya WATOTO chini ya Umri wa Miaka Mitano.

Katika harakati za kuhakikisha vifo vya akina mama vinaendelea kupungua kila Mwaka Tarehe 05 ya Mwezi Mei ni Siku ya Wakunga Duniani.ambayo huadhimishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) , Kwakushirikiana na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) na wadau wengine wa Afya ya Mama na Mtoto.

Maadhimisho haya  kwa mmwaka huu yatafanyika katika Mkoa wa Morogoro 05 Mei 2018 na Mgeni Rasmi katika Maadhimisho haya ni Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambapo kauli Mbiu ya Mwaka huu ni 'MKUNGA NI KIONGOZI KATIKA UTOAJI WA HUDUMA BORA KWA MAMA NA MTOTO'.

Madhumuni ya Maadhimisho haya ni Kutoa hamasa kwa watunga Sera na Watoa Maamuzi ili Kuhakikisha Kwamba rasilimali muhimu zinakuwepo kwa ajili ya WAKUNGA lakini pia kutambua nafasi ya Pekee waliyonayo wakunga wenye taaluma katika Jamii. bwarren@unfpa.org

Post a Comment

Previous Post Next Post