Mbunge wa Misungwi pia aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga amesema kama Waziri wa Fedha, Dk Philip Mpango hana haja yakuendelea kuwa kuwepo kwenye wizara hiyo kama anasema hakuna fedha
Kitwanga amesema hayo leo bungeni leo jioni Alhamisi Mei 24, 2018 katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Nishati mwaka 2018/19.
"Hivi kwanini unakosa fedha? Kama ni waziri wa fedha halafu unasema
hakuna fedha ondoka hapo,” amesema.
Kitwanga amesema miradi midogo ina gharama kubwa za uendeshaji ikiwemo kuwalipa mishahara watumishi wanaohudumia katika vituo hivyo na kumshauri Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani kuja na mpango wa kuzalisha umeme wa Megawati 5,000 kwa kutumia makaa ya mawe.
“Wazungu wanasema uzalishaji wa umeme kwa kutumia makaa ya mawe unachafua hali ya hewa lakini wao wanazalisha umeme kwa kutumia makaa hayo kwa sababu teknolojia imebadilika,” amesema.
“Duniani kote umeme wa bei nafuu ni unaozalishwa na maji ama
Makaa.”
