Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetaja viingilio vya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2017/2018 kati ya Simba na Yanga utakaochezwa Mei 29 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Katika mchezo huo namba 178 utakaofanyika Saa 10:00 jioni, kiingilio cha chini kitakuwa shilingi 7,000 wakati kiingilio cha juu kitakuwa shilingi Elfu Thelathini.
Jukwaa la VIP A itakuwa shilingi Elfu Thelathini (30,000),VIP B na C shilingi Elfu Ishirini (20,000) na Upande wa Mzunguko kwenye viti vya rangi ya Chungwa,Bluu na Kijani itakuwa shilingi Elfu Saba (7,000)
Tiketi tayari zimeanza kupatikana kuanzia sasa kupitia Selcom
