Kifo cha mdogo wa Heche chamuibua Ridhiwan Kikwete


Mbunge wa Chalinze, Ridhiwan Kikwete amelaani mauji ya Ndugu wa Mbunge wa Tarime John Heche kinachodaiwa kutekelezwa na mmoja wa askari wa jeshi la Polisi Mkoani Mara.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi tayari askari huyo yupo chini ya ulinzi ili kuchukuliwa hatua za kisheria zaidi.

Ridhiwan kupitia kwenye kurasa yake ya mtabdao wa Instagram ameweka ameweka picha na kusema kuwa kitendo hicho sio cha kufumbiwa macho.

"Kitendo kilichotokea si tu kimesikitisha Ukoo wa Bwana Heche lakini kwangu Binafsi. Jeshi letu limetengenezwa kulinda watu na Mali zao si kuumiza wasio na hatia. Imani yangu Serikali itasimamia haki kwa familia ya Heche. Poleni sana kwa Msiba.Mungu awape subira," ameandika Ridhiwan Kikwete

Post a Comment

Previous Post Next Post