Rais wa Tanzania John Magufuli leo Aprili 26, 2018 ametangaza rasmi kuwa Manispaa ya Dodoma kuwa jiji.
Ameyasema hayo leo mjini Dodoma akihutubia katika sherehe za maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano zilizofanyika katika Uwanja wa Jamhuri mjini humo.
"Kuanzia leo kwa mamlaka mlionipa watanzania Dodoma ni jiji kwahiyo maangalizi yote ya kisheria yaanze na Mkurugenzi wa manispaa aliyekuwepo hapa anakuwa Mkurugenzi wa jiji la Dodoma," amesema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli amesisitiza kuwa adhma ya Serikali kuhamia Dodoma ipo pale pale ambapo zaidi ya watumishi 3800 wa serikali wameshahamia Dodoma na ameahidi kuwa mwaka huu atahamia mjini humo.