Katika hali iloyochukua vichwa vya habari mjini ni kuhusu Staa wa muziki Tanzania, Zuwena Mohamed “Shilole” baada ya kusema kuwa hatachora tena tatoo ya mwanaume baada ya kucjora ya mumewe wa sasa Uchebe.
Shilole ameamua kuachia picha kupitia akaunti yake ya instagram na kuonyesha tattoo mpya aliyoichora kwenye mwili wake kwa kuandika jina la 'Ashirafu' ambaye ni maarufu kama Uchebe na kuandika maneno haya “Kwa mara ya kwanza na ya mwisho nimechora tatooooo ya jina la mume wangu Nampendaa sana”
Shilole alishawahi pia kuchora tattoo ya aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Nuh Mziwanda na baadae kuifuta na hii itakuwa tattoo yake ya pili kuichora lenye jina la mwanaume ambae ni mpenzi wake na kuionyesha hadharani.

